Tuesday, 13 January 2026

Begginer Dialogues


DIALOGUE: PICKING A FRIEND & VISITING A WOMEN’S PROJECT
(Practice: “TO HAVE” – KUWA NA)

SWAHILI

Mgeni: Habari.
Rafiki: Nzuri. Karibu.
Mgeni: Asante. Una muda sasa?
Rafiki: Ndiyo, nina muda.
Mgeni: Nina mpango wa kwenda kwenye mradi wa wanawake.
Rafiki: Sawa. Mradi una watu wangapi?
Mgeni: Una wanawake kumi.
Rafiki: Mradi una chakula?
Mgeni: Ndiyo, una chakula cha kienyeji.
Rafiki: Sawa. Twende.

(baada ya kufika)

Mwanamke wa Mradi: Karibu sana.
Mgeni: Asante.
Mwanamke wa Mradi: Tuna mradi wa wanawake.
Rafiki: Mnafanya nini hapa?
Mwanamke wa Mradi: Tunaandaa chakula endelevu.
Mgeni: Mna chakula gani?
Mwanamke wa Mradi: Tuna wali, mboga na samaki.
Rafiki: Mna wateja?
Mwanamke wa Mradi: Ndiyo, tuna watalii wengi.
Mgeni: Mradi una manufaa kwa jamii.
Mwanamke wa Mradi: Ndiyo, una msaada kwa wanawake.
Mgeni: Nina furaha kuwa hapa.
Mwanamke wa Mradi: Asante sana.


ENGLISH

Visitor: Hello.
Friend: Hello. Welcome.
Visitor: Thank you. Do you have time now?
Friend: Yes, I have time.
Visitor: I have a plan to go to a women’s project.
Friend: Okay. How many people does the project have?
Visitor: It has ten women.
Friend: Does the project have food?
Visitor: Yes, it has local food.
Friend: Okay. Let’s go.

(after arriving)

Woman at the Project: You are very welcome.
Visitor: Thank you.
Woman at the Project: We have a women’s project.
Friend: What do you do here?
Woman at the Project: We prepare sustainable food.
Visitor: What food do you have?
Woman at the Project: We have rice, vegetables and fish.
Friend: Do you have customers?
Woman at the Project: Yes, we have many tourists.
Visitor: The project has benefits for the community.
Woman at the Project: Yes, it supports women.
Visitor: I am happy to be here.
Woman at the Project: Thank you very much.

FOLLOW-UP DIALOGUE: BUYING FOOD
(Practice: “TO HAVE” – KUWA NA)

SWAHILI

Mgeni: Habari.
Mwanamke wa Mradi: Habari, karibu.
Mgeni: Nina njaa.
Mwanamke wa Mradi: Tuna chakula kizuri.
Mgeni: Mna chakula gani leo?
Mwanamke wa Mradi: Tuna wali na mboga.
Mgeni: Chakula kina bei gani?
Mwanamke wa Mradi: Ni shilingi elfu tano.
Mgeni: Nina pesa taslimu.
Mgeni: Una chenji?
Mwanamke wa Mradi: Ndiyo, nina chenji.
Mgeni: Sawa, ninachukua chakula.
Mwanamke wa Mradi: Asante sana.
Mgeni: Asante.


ENGLISH

Visitor: Hello.
Woman at the Project: Hello, welcome.
Visitor: I am hungry.
Woman at the Project: We have good food.
Visitor: What food do you have today?
Woman at the Project: We have rice and vegetables.
Visitor: How much is the food?
Woman at the Project: It is five thousand shillings.
Visitor: I have cash.
Visitor: Do you have change?
Woman at the Project: Yes, I have change.
Visitor: Okay, I’ll take the food.
Woman at the Project: Thank you very much.
Visitor: Thank you.



Friday, 9 January 2026

Begginer Dialogues


DIALOGUE 1: AIRPORT (IMMIGRATION)

SWAHILI

Afisa wa Uhamiaji: Habari, karibu.
Mgeni: Habari.
Afisa wa Uhamiaji: Jina lako nani?
Mgeni: Jina langu ni ______.
Afisa wa Uhamiaji: Unatoka nchi gani?
Mgeni: Ninatoka ______.
Afisa wa Uhamiaji: Unakuja Tanzania kwa nini?
Mgeni: Ninakuja kwa likizo.
Afisa wa Uhamiaji: Utakaa Tanzania kwa muda gani?
Mgeni: Nitakaa wiki mbili.
Afisa wa Uhamiaji: Unakaa wapi?
Mgeni: Nitakaa hotelini.
Afisa wa Uhamiaji: Una familia au rafiki hapa?
Mgeni: Ndiyo, nina rafiki hapa.
Afisa wa Uhamiaji: Sawa. Karibu Tanzania.
Mgeni: Asante sana.


ENGLISH

Immigration Officer: Hello, welcome.
Visitor: Hello.
Immigration Officer: What is your name?
Visitor: My name is ______.
Immigration Officer: Which country are you coming from?
Visitor: I am coming from ______.
Immigration Officer: Why are you coming to Tanzania?
Visitor: I am coming for a holiday.
Immigration Officer: How long will you stay in Tanzania?
Visitor: I will stay for two weeks.
Immigration Officer: Where will you stay?
Visitor: I will stay at a hotel.
Immigration Officer: Do you have family or a friend here?
Visitor: Yes, I have a friend here.
Immigration Officer: Okay. Welcome to Tanzania.
Visitor: Thank you very much.


==========================
DIALOGUE 2: HOTEL (CHECK-IN)

SWAHILI

Mhudumu wa Hoteli: Habari, karibu hotelini.
Mgeni: Habari.
Mhudumu wa Hoteli: Jina lako nani tafadhali?
Mgeni: Jina langu ni ______.
Mhudumu wa Hoteli: Una booking?
Mgeni: Ndiyo, nina booking.
Mhudumu wa Hoteli: Ume-book kwa siku ngapi?
Mgeni: Nime-book kwa siku kumi na nne.
Mhudumu wa Hoteli: Chumba kimoja au viwili?
Mgeni: Chumba kimoja tafadhali.
Mhudumu wa Hoteli: Hiki ni chumba chako.
Mhudumu wa Hoteli: Hii ni funguo yako.
Mgeni: Asante sana.
Mhudumu wa Hoteli: Kama una swali, tafadhali uliza.
Mgeni: Sawa, asante.


ENGLISH

Hotel Receptionist: Hello, welcome to the hotel.
Guest: Hello.
Hotel Receptionist: What is your name please?
Guest: My name is ______.
Hotel Receptionist: Do you have a booking?
Guest: Yes, I have a booking.
Hotel Receptionist: How many days have you booked?
Guest: I have booked for fourteen days.
Hotel Receptionist: One room or two?
Guest: One room please.
Hotel Receptionist: This is your room.
Hotel Receptionist: This is your key.
Guest: Thank you very much.
Hotel Receptionist: If you have a question, please ask.
Guest: Okay, thank you.


==========================
DIALOGUE 3: RESTAURANT

SWAHILI

Mhudumu: Karibu.
Mgeni: Asante.
Mhudumu: Unaweza kukaa hapa.
Mgeni: Sawa.
Mhudumu: Ungependa kula nini?
Mgeni: Ningependa chakula cha Kitanzania.
Mhudumu: Tuna wali, ugali, samaki na kuku.
Mgeni: Nataka wali na kuku.
Mhudumu: Unataka kunywa nini?
Mgeni: Nataka maji, tafadhali.
Mhudumu: Sawa.
Mhudumu: Chakula kiko tayari.
Mgeni: Asante.
Mhudumu: Chakula ni kizuri?
Mgeni: Ndiyo, ni kizuri sana.
Mgeni: Naomba bili.
Mhudumu: Hii hapa.
Mgeni: Asante sana.


ENGLISH

Waiter: Welcome.
Guest: Thank you.
Waiter: You can sit here.
Guest: Okay.
Waiter: What would you like to eat?
Guest: I would like Tanzanian food.
Waiter: We have rice, ugali, fish and chicken.
Guest: I want rice and chicken.
Waiter: What would you like to drink?
Guest: I want water, please.
Waiter: Okay.
Waiter: The food is ready.
Guest: Thank you.
Waiter: Is the food good?
Guest: Yes, it is very good.
Guest: May I have the bill?
Waiter: Here it is.
Guest: Thank you very much.


==========================
DIALOGUE 4: SHOP / MARKET

SWAHILI

Muuzaji: Karibu.
Mgeni: Asante.
Muuzaji: Unatafuta nini?
Mgeni: Natafuta zawadi.
Muuzaji: Unataka zawadi ya aina gani?
Mgeni: Nataka zawadi ndogo.
Muuzaji: Hii ni nzuri sana.
Mgeni: Bei gani?
Muuzaji: Ni shilingi elfu kumi.
Mgeni: Ni ghali kidogo.
Muuzaji: Sawa, elfu nane.
Mgeni: Sawa.
Mgeni: Asante.
Muuzaji: Asante, karibu tena.


ENGLISH

Shopkeeper: Welcome.
Visitor: Thank you.
Shopkeeper: What are you looking for?
Visitor: I am looking for a gift.
Shopkeeper: What kind of gift do you want?
Visitor: I want a small gift.
Shopkeeper: This one is very nice.
Visitor: How much is it?
Shopkeeper: It is ten thousand shillings.
Visitor: It is a bit expensive.
Shopkeeper: Okay, eight thousand.
Visitor: Okay.
Visitor: Thank you.
Shopkeeper: Thank you, welcome again.


==========================
DIALOGUE 5: TAXI / TRANSPORT

SWAHILI

Dereva wa Teksi: Habari.
Mgeni: Habari.
Dereva wa Teksi: Unakwenda wapi?
Mgeni: Naenda hotelini.
Dereva wa Teksi: Hoteli gani?
Mgeni: Hoteli ya ______.
Dereva wa Teksi: Iko wapi?
Mgeni: Iko karibu na katikati ya mji.
Dereva wa Teksi: Sawa.
Dereva wa Teksi: Ni watu wangapi?
Mgeni: Mtu mmoja.
Dereva wa Teksi: Safari itachukua dakika ishirini.
Mgeni: Sawa.
Dereva wa Teksi: Bei ni shilingi elfu ishirini.
Mgeni: Ni ghali kidogo.
Dereva wa Teksi: Sawa, elfu kumi na tano.
Mgeni: Sawa.
Dereva wa Teksi: Uko tayari?
Mgeni: Ndiyo, niko tayari.
Dereva wa Teksi: Twende.


ENGLISH

Taxi Driver: Hello.
Visitor: Hello.
Taxi Driver: Where are you going?
Visitor: I am going to the hotel.
Taxi Driver: Which hotel?
Visitor: ______ Hotel.
Taxi Driver: Where is it?
Visitor: It is near the city center.
Taxi Driver: Okay.
Taxi Driver: How many people?
Visitor: One person.
Taxi Driver: The trip will take twenty minutes.
Visitor: Okay.
Taxi Driver: The price is twenty thousand shillings.
Visitor: It is a bit expensive.
Taxi Driver: Okay, fifteen thousand.
Visitor: Okay.
Taxi Driver: Are you ready?
Visitor: Yes, I am ready.
Taxi Driver: Let’s go.