Friday, 23 February 2024

Shule Yatatua Tatizo la Fedha

Katika mji wa St. Mary’s, shule ya Kikatoliki inayosimamiwa na masista wenye bidii ilikumbana na changamoto za kifedha. Masista hawangeweza kuwaomba wazazi waongeze pesa na walimu hawakulipwa kwa wakati. Masisita na walimu walifahamu hali ngumu za wazazi na kwa hiyo, walijadili njia za kupunguza mzigo.

Ili kukabiliana na hali hiyo, jamii ilipanga kuchangisha pesa. Wafanya-biashara na wazazi walitoa michango yao. Kwa sababu ya umoja wa watu na kujitolea, shule ilipata matumaini.

Masisita wa Kikatoliki na jamii walijiunga pamoja kuhakikisha eliu inaaendelea katika shule hiyo. Juhudi zao za pamoja zilionyesha kwamba, hata wakati hali ni ngumu; walimu, wanafunzi na jamii, wote wanaweza kuungana na kutatua matatizo ambayo wanapitia.

Kutokana na juhudi za kuchangisha pesa, shule ya St. Mary’s ilipata mabadikilko mazuri. Walimu walipokea mishahara hao iliyokuwa imechelewa. Wanafunzi nao walifaidika kwa kupata vitabu vipya na madarasa bora, wafadhili wakarimu walifurahishwa na matokeo mazuri ya michango yao.

Barua za shukrani kutoka kwa wanafunzi na walimu ziliimarisha uhusiano kati ya shule na wafadhili wake. Sasa, wakati ujaoo wa shule ulionekana kuwa wenye matumaini zaidi kwa sababu ya juhudi za wote waliohusika.

Ziara ya Zuri

Mwaka uliopita, mwezi wa Septemba, mwanamke mkarimu ambaye anaitwa Zuri pamoja na mvulana wake, walisafiri kutoka Uingereza hadi Kenya. Zuri alinunua mashine mbili za kushona na aliwafundisha wanawake na wasichana jinsi ya kutengeneza pedi au sodo. Zuri alienda kwenye shule ya wasichana na kuwapa wanafunzi vitabu, kalamu na vitu vya kuchorea. Wasichana walifurahi sana na hata waliimba nyimbo za kumshukuru.

Mwanamke mmoja wa Kimaasai alimpa Zuri bangili nzuri na mkufu ambao ulitengenezwa kwa shanga. Wanawake wengine katika kijij hicho pia walimpa zawadi maridadi.

Zuri hakula chakula cha kawaida cha Kimaasai. Badala yake, wanawake wa eneo hilo walitayarisha mandari au kwa jina lingine, pikniki kwa chakula cha mchana. Walileta vitu vitamu kama samosa, chapati, saladi, chai, keki , sandiwichi na matunda. Wote walifurahia sana.

Zuri alikaa Kenya kwa wiki mbili na siku moja akitembelea maeneo tofauti. Hata alifanya kazi na wanawake waliokuwa gerezani. Kando na kushona, pia alishiriki hadithi na kujifunza kutoka kwa wengine.

Zuri hakuishi mahali pake pa kawaida kwa sababu kulikuwa na wageni. Aliishi katika eneo tofauti. Alikaa pamoja na mvulana wake. Ingawa safari ilikuwa ya kuchosha, Zuri na mvulana wake waliifurahia sana.