Mwaka uliopita, mwezi wa Septemba, mwanamke mkarimu ambaye anaitwa Zuri pamoja na mvulana wake, walisafiri kutoka Uingereza hadi Kenya. Zuri alinunua mashine mbili za kushona na aliwafundisha wanawake na wasichana jinsi ya kutengeneza pedi au sodo. Zuri alienda kwenye shule ya wasichana na kuwapa wanafunzi vitabu, kalamu na vitu vya kuchorea. Wasichana walifurahi sana na hata waliimba nyimbo za kumshukuru.
Mwanamke mmoja wa Kimaasai
alimpa Zuri bangili nzuri na mkufu ambao ulitengenezwa kwa shanga. Wanawake
wengine katika kijij hicho pia walimpa zawadi maridadi.
Zuri hakula chakula cha
kawaida cha Kimaasai. Badala yake, wanawake wa eneo hilo walitayarisha mandari
au kwa jina lingine, pikniki kwa chakula cha mchana. Walileta vitu vitamu kama
samosa, chapati, saladi, chai, keki , sandiwichi na matunda. Wote walifurahia
sana.
Zuri alikaa Kenya kwa wiki
mbili na siku moja akitembelea maeneo tofauti. Hata alifanya kazi na wanawake
waliokuwa gerezani. Kando na kushona, pia alishiriki hadithi na kujifunza
kutoka kwa wengine.
Zuri hakuishi mahali pake pa
kawaida kwa sababu kulikuwa na wageni. Aliishi katika eneo tofauti. Alikaa
pamoja na mvulana wake. Ingawa safari ilikuwa ya kuchosha, Zuri na mvulana wake
waliifurahia sana.
No comments:
Post a Comment