Friday, 26 September 2025

Kiswahili Quiz – Intermediate Level

Section A: Grammar & Structures

1. Negations – Badilisha sentensi hizi kuwa kinyume (negative):

  1. Nina kaka mmoja.

  2. Wanafunzi wanakimbia uwanjani.

  3. Tunakunywa maji.

  4. Mama anaenda sokoni.

  5. Mtoto amelala.

2. “TO BE” – (kuwa) – Jaza nafasi:

  1. Mimi ___ mwanafunzi. (present tense)

  2. Wewe ___ dada yangu. (past tense)

  3. Sisi ___ marafiki. (future tense)

  4. Yeye ___ mgonjwa. (past perfect tense)

  5. Wao ___ walimu. (present tense)

3. “TO HAVE” – (kuwa na) – Tafsiri kwa Kiswahili:

  1. She has a house.

  2. We had many books.

  3. I have a good friend.

  4. They will have two cars.

  5. He has a dog.

4. Numbers & Time

  1. Andika saa kwa Kiswahili: 4:15 pm

  2. Andika nambari kwa Kiswahili: 237

  3. Andika nambari kwa Kiswahili: 1,045

  4. Je, siku moja ina saa ngapi?

  5. Andika kwa Kiswahili: 19th January

5. Demonstratives – Tafsiri:

  1. This is my book.

  2. Whose pen is that?

  3. Those shirts are yours.

  4. Who is this?

  5. Whose dress is this?


Section B: Vocabulary & Communication

6. Greetings (Colloquial Chp. 1)
Tengeneza mazungumzo mafupi kati ya watu wawili wanaokutana mara ya kwanza:

_________________________________
_________________________________
_________________________________
_________________________________

7. Colors
Taja rangi tatu unazopenda:

  1. ___________________
  2. ___________________
  3. ___________________

8. Hisia (Feelings) – Jibu maswali kwa Kiswahili:

  1. Una hisi vipi leo?

  2. Unapokuwa na huzuni, unafanya nini?

  3. Ni wakati gani unahisi furaha zaidi?

  4. Je, rafiki yako anapokuwa na hasira, unamshauri nini?

  5. Ni jambo gani linakufanya uogope?

9. Foods / Recipes

a) Taja vyakula vitatu unavyopenda kula nyumbani:

  1. ___________________
  2. ___________________
  3. ___________________

b) Andika hatua za kupika wali kwa Kiswahili:
_________________________________
_________________________________

10. Possessives – Jaza nafasi:

  1. Hii ni kalamu ______ (langu / yangu).

  2. Hizo ni vitabu ______ (vyetu / wetu).

  3. Hii ni nyumba ______ (yake / zake).

  4. Hawa ni marafiki ______ (wangu / yangu).

  5. Hizi ni nguo ______ (zake / yake).


Section C: Reading Comprehension

Soma kifungu kifuatacho, kisha jibu maswali:

Kusherehekea Siku ya Kuzaliwa ya Dadangu
Jumamosi tutasherehekea siku ya kuzaliwa ya dadangu Amina. Atafikisha miaka ishirini na mitano. Asubuhi tutapamba nyumba kwa mapambo mazuri. Mama atapika wali na kuku, na kaka yangu ataleta keki kubwa yenye mishumaa. Wakati wa mchana marafiki wa Amina watakuja. Dada yangu atakata keki na kugawa vipande kwa kila mtu. Tutacheza muziki na michezo hadi jioni. Itakuwa siku ya furaha sana kwa familia yetu.

Maswali:

  1. Ni nani atasherehekea siku ya kuzaliwa?

  2. Amina atatimiza miaka mingapi?

  3. Mama atapika chakula gani?

  4. Ni akina nani watakuja?

  5. Eleza kwa sentensi moja jinsi familia itakavyohisi siku hiyo.


No comments:

Post a Comment